Jumatatu , 26th Apr , 2021

Mcheza kikapu nyota wa Brooklyn Nets, Kevin Durant amerejea dimbani dhidi ya Phoenix Suns usiku wa kuamkia leo na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa alama 128-119 kwenye ligi kuu ya kikapu nchini Marekani NBA tokea awe nje ya uwanja Aprili 7, 2021.

Kevin Durrant akimtoka mlinzi wa Phoenix Suns usiku wa kuamkia leo.

Durrant aliyekosa michezo 23 kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli, amerejea na kucheza dakika 28 ambapo amekuisanyia timu yake alama 33, rebaundi 6 na assisti 4 na kumfanya kuwa mchezaji watatu aliyekusanya alama nyingi nyuma ya Devin Booker na Kyrie Iriving.

Booker ameibuka nyota wa mchezo kwa kupata alama 36, rebaundi 3 na assisti 1 na wapili akiwa mchezaji mwenzake wa Brooklyn Nets, Kyrie Iriving aliyeibuka na alama 34, rebaudi 6 na assisti 12.

Durrant ameonekana mwenye furaha baada ya kurejea dimabani huku akijinasibu kuwa, ubora anaouonesha ni kitu cha kawaida wasababu ukijua kucheza mpira wa kikapu ni sawa  na kujua kuendesha baiskeli kwa maan aya kwamba ukijua umejua pamoja na kusifu wachezaji wenzake.

Durrant baada ya kurejea amesema, “Ni kama kuendesha baiskeli tu, unahitaji kuweka miguu yako sawa na kuzidi kuendelea kucheza na anafikiri wachezaji wenzangu wamefanyakazi kubwa ya kucheza na mimi muda wote”.

Ushindi huo umeifanya Brooklyn Nets kukwea kileleni mwa msimamo wa NBA kwa upande wa mashariki na kuishusha nafasi ya pili Philadelphia 76ers.