Alhamisi , 17th Feb , 2022

Uwanja wa Molinuex unaomilikiwa na klabu ya Wolverhampton umechaguliwa na Shirikisho la Soka nchini England kutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya taifa England kwenye michezo miwili ijayo ya michuano ya UEFA Nations League.

(Kikosi cha timu yataifa ya England 2022)

England inataraji kucheza dhidi ya Italia ‘Azzuri’ Jumamosi ya Juni 11, 2022 na Hungary Jumanne ya Juni 14 mwaka huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu Disemba 1956.

Akiongelea suala hili la uwanja, Kocha wa England, Gareth Southgate amesema " Wembley ni nyumbani lakini furaha kwetu ni kuanza safari ya michuano mikubwa kwenye uwanja wenye historia kubwa”.

Mchezo wa Italia dhidi ya England utachezwa bila ya mashabiki kufuatia agizo la UEFA la kuzuia mashabiki kutokana na vurugu za mashabiki zilizojitokeza kwenye mchezo wa fainali ya Michuano ya EURO mwaka jana kati ya England dhidi ya Italia.

England ipo kundi A3 katika michuano hiyo pamoja na timu za Italia, Hungary na Ujerumani.

Michezo ya makundi ya michuano ya UEFA Nations League inatarajiwa kumalizika mwezi Septemba 2022 kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la Dunia Novemba 2022 nchini Qatar.