Jumanne , 14th Dec , 2021

EPL inarejea tena usiku wa leo Disemba 14, 2021 mzunguko wa 17 kwa michezo miwili kuchezwa baina ya Norwich City dhidi ya Aston villa saa 4:45 usiku ilhali   Manchester City dhidi ya Leeds United saa 5:00 usiku.

(Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo)

Mchezo uliopaswa kuchezwa usiku wa leo kati ya Manchester United dhidi ya Brentford uliopaswa kuchezwa leo umehairishwa kutokana na mambukizi ya Uviko 19 katika viunga vya Old Traffod.

Bodi ya EPL imesema “Tumeamua kufuata ushauri wa wataalamu kuhusu mazingira tuliyonayo kwa sasa na hivyo Bodi ya ligi tumeamua kuchukua uamuzi wa kuhairisha mchezo kwa kufuata ushauri wa madaktari”.

Visa 42 vya maambukizi vya Uviko-19 vimeripotiwa kwa wachezaji na maafisa wa timu ndani ya wiki moja ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya visa kuripotiwa tangu kuzuka kwa janga hilo may 2020

Bodi imesisitiza sasa kutakuwa na vipimo vya mara kwa mara kwa wachezaji na maafisa wa vilabu ili kupambana na mambukizi ya uviko 19 Huku vilabu vya Brighton, Tottenham, Leicester, Aston Villa na Norwich vikithibitisha kuwa na maambukizi kwa baadhi ya wachezaji na maafisa wa timu zao.