Alhamisi , 12th Mar , 2015

Michuano ya Ligi ya Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es salaam inatarajia kufikia tamati yake hapo kesho kwa kuchezwa fainali ya wanaume kati ya JKT na Savio huku wanawake zikiwakutanisha Jeshi Stars na Don Bosco Lioness, Uwanja wa ndani wa Taifa.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa Chama cha mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, Richard Julles amesema fainali hizo zitatanguliwa na mechi za kutafuta mshindi wa tatu kwa upande wa timu za wasichana ambapo watakutana na timu zitakazowakutanisha timu ya Tanzania Prisons ikicheza na Jeshi stars huku mshindi wa tatu kwa wanaume zikicheza timu za Pazi na Vijana.

Julles amesema, michuano hiyo imekuwa na changamoto mbalimbakli hususani katika ushindani baina ya timu na timu suala ambalo lilichangia kila timu kujitahidi katika mazoezi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri katika michuano hiyo.