Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Taifa Stars ilikubali kichapo cha mabao 2-0, yaliyofungwa na straika huyo huku akiwa ndiye mchezaji pekee aliyeweza kubadilishana jezi na mchezaji wa Stars.
Baada ya zoezi hilo Farid alisema Mohamed ndiye alikwenda kumuomba wabadilishane jezi kitendo kilichokubaliwa na kiungo huyo anayetarajia kujiunga na Klabu ya Teneriffe, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.
Farid amesema hakuwa na mpango wa kubadilishana jezi na mchezaji yeyote lakini alipofuatwa na Salah na kuombwa alikubali ombi lake.
"Kukweli kwanza sikupanga kubadilishana jezi na mchezaji yoyote, lakini aliponifuata Salah nikiwa sina jinsi nikakubali kumpa jezi yangu naye akanipa yake," alisema Farid ambaye alionyesha kiwango cha juu kwenye mechi hiyo.



