
Washindi wa SportPesa Super Cup wakishangilia Kombe lao
Kwa ushindi huo Gor Mahia inajinyakulia zawadi ya dola elfu 30 ($ 30,000) huku ikisubiri kuja kucheza na Everton ya nchini Uingereza July 13 jijini Dar es salaam.
Mchezo huu umeifanya Gor Mahia kuvunja rekodi waliyojiwekea wenyewe katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Sportpesa kwa kuwa timu iliyoongoza kupata magoli mengi kuliko timu zote zilizoshiriki michuano hiyo huku ikikomaa kumaliza michezo yake ndani ya dakika 90 uwanjani.
Ushindi wa Gor Mahia umetangazwa na wachezaji watatu walioweza kutingisha nyavu za mashemeji zao ambao ni Otieno Timothy, Oliver Maluba na John Ndirangu, huku mchezaji Medie Kagere akichukua kiatu cha mfungaji bora wa michuano hiyo.
Kwenye michuano hii Gor Mahia imeonyesha ubabe wake ambapo tangu ilipoanza Jumatatu ya wiki hii imeweka kwapani goli saba bila kukubali kufungwa na timu zote walizokutana nazo.
Gor Mahia wakishangilia ushindi wakiwa na Kombe lao