Jumatatu , 24th Jan , 2022

Nyota wa tennis kutoka Romania Simona Halep ametupwa nje ya michuano ya wazi ya Australia kwa mwaka 2022 baada ya kufungwa katika seti tatu na Mfaransa Alize Cornet na kuungana na nyota wakubwa duniani waliotupwa nje kama Naomi Osaka, Emma Raducanu,Petra Kvitova katika michuano hiyo.

Daniil Medvedev.

Halep anayekamata nafasi 14 kwa viwango vya ubora duniani alipoteza kwa seti 6-4 3-6 6-4 dhidi ya Cornet anayekamata nafasi ya 61 kwa viwango vya ubora huku nyota huyo sasa atapambana na nyota kutoka Marekani Danielle Collins  anayekamata nafasi ya 27 kwa ubora duniani.

Ilhali upande wa wanaume Mrusi Daniil Medvedev ametinga hatua ya robo fainali baada ya kumfunga Mmarekani Maxime Cressy kwa seti 6-2 7-6 (7-4) 6-7 (4-7) 7-5 huku sasa akipambana na Mcanada Felix Auger-Aliassime anayekamata nafasi ya 9 ambaye alimuondoa Mcroatia Marin Cilic anayekamata nafsai ya 27 kwa ubora duniani

Medvedev ambaye alitwaa ubingwa wa wazi wa Marekani kwa mwaka 2021 baada ya kumfunga Novak Djokovic mwezi september anasalia kuwa kinara kwenye nyota wanopigiwa chapuo la kutwaa taji hilo sambamba na nyota kutoka nchini Hispania Rafael Nadal.