Hapatoshi VPL leo Mbeya City, Ruvu Shooting

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Mbeya City inaikaribisha Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu leo Tanzania, bara itakayofanyika katika uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya ambayo inatafsiriwa ni kama kisasi.

Mbeya City wakiwa mazoezini

Katika mechi ya kwanza 15/11/2020 Ruvu Shooting akiwa nyumbani aliibuka na ushindi wa 3-0, hali inayoifanya mechi hii kuwa katika uzito wa juu na pia nafasi aliyopo Mbeya City si salama sana kusalia katika katika ligi kuu .

Kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo huu katika uwanja wa Sokoine asubuhi ya leo, timu zote mbili zimetumia muda kutambiana kwamba kila moja itaibuka na ushindi, mwenyeji wakitamba kupata alama zote tatu muhimu, na mgeni akiziwinda alama hizi kwa udi na uvumba.

Mbeya City timu iliyopanda ligi kuu mwaka 2012 na kuja kutoa upinzani wa hali ya juu,ipo katika wakati mgumu kwa sasa ikipamba kusalia katika ligi kuu.

Ligi kuu Tanzania bara inashirikisha timu 18, ambazo timu 4 zilizoshika nafasi ya (18,17,16,15) zitashuka daraja moja kwa moja, huku zile zilizoshika nafasi ya 14 na 13 zitacheza mechi za mtoano 'Play Off' na timu za daraja la kwanza.

Takwimu za Mbeya City katika msimu huu michezo 30 , kushinda 6 sare 12, 10 kupoteza magoli ya kufunga 20 ya kufungwa 27 bafasi katika msimamo ni 15.