Jumamosi , 14th Sep , 2019

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, amesema kitendo cha Zesco United kusawazisha hakijabadili chochote kwa timu yake kwani hata kama wangeshinda leo bado wangehitajika kufunga goli ugenini.

Wachezaji wa Yanga na Zesco kwenye mechi ya leo

Zahera amesema hayo leo Septemba 14, 2019 baada ya mchezo wa kwanza wa hatua za awali kuwania kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ambao umeisha kwa sare ya goli 1-1.

''Hakuna kilichobadilika hata kama wamefunga na sisi tunapaswa kwenda kufunga kule Zambia na hata kama wasingefunga bado tulipaswa kwenda kufunga goli kwahiyo tutahakikisha tunafunga kwao'', - Zahera.

Mchezo wa marudiano utapigwa Septemba 27 huko Lusaka Zambia, ambapo mshindi wa jumla atasonga mbele katika hatua ya makundi.