
Kocha Msaidizi wa Simba, Hiitmana Thierry (kushoto) na Kocha mpya wa klabu hiyo, Pablo Franco (kulia).
Hitimana amesema, “Nimefurahi kukutana naye naamini huu ni wakati wa kumpa muda na ushirikiano ili aweze kuitoa Simba mahala ilipo na kuipeleka mbele zaidi kama alivyofanya mtangulizi wake”.
Hitimana ameyasema hayo kocha mpya wa Simba, Pablo Franco alipowasili nchini Novemba 10, 2021 na kutembelea kambi ya wachezaji na Uongozi wa klabu hiyo maeneo ya Bunju pembeni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.