Jumatatu , 3rd Dec , 2018

Klabu ya soka ya Simba leo, Disemba 3, 2018 imefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya wenyeji wao Mbabane Swallows kesho huko mjini Manzini eSwatini.

Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi.

Mazoezi hayo ya mwisho yamefanyika kwenye uwanja wa Mavuso Sports Centre, ambao ndio utatumika kwa mchezo huo. Uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki 5,000 tu.

Taarifa ya klabu ya Simba kutoka manzoezini imeeleza kuwa wamefanikiwa kumaliza mazoezi hayo salama hivyo wapo tayari kwaajili ya mchezo huo.

''Wachezaji wetu wamefanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ambao utachezwa kesho Jumanne Desemba 4, 2018'', aimeeleza taarifa hiyo.

Simba wapo mbele kwa mabao 4-1, ushindi walioupata wiki moja iliyopita kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hivyo watakuwa na kazi ndogo ya kulinda ushindi kupitia kuzuia kufungwa au wao kuongeza magoli.