Jumatano , 20th Jan , 2021

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya klabu ya Azam imemteua Nassor Idrissa Mohamed almaarufu ‘Father’ kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kuanzia leo tarehe 19 Januari 2021 kuchukua nafasi ya Shani Christoms ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria na Utawala kwasasa.

Idrissa Nassor mwenyekiti mpya wa klabu ya Azam.

Kabla ya uteuzi huo, Nassor Idrissa alikuwa akihudumu kama mkurugenzi mshauri wa klabu Azam na miaka ya nyuma kuanzia mwaka 2016 aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kuchukua nafasi ya Alhaji Said Mohamed Abeid aliyefariki mapema mwezi novemba 2016.

Kabla ya kupandishwa cheo na bodi ya wakurugenzi wa Azam kuwa mwenyekiti wao kuchukua nafasi ya marehemu Alhaji Said Mohamed Abeid mwaka 2016, Nassor Idrissa alikuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo hivyo amedumu zaidi ya miaka 4 klabuni hapo.