Jumatano , 7th Mei , 2025

Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini maarufu kama Msukuma amelivalia njuga sakata la dabi ya Kariakoo leo bungeni Jijini Dodoma akitaka shirikisho la Soka hapa Nchini Kuunda bodi ya Ligi nyingine iliyo huru ili kutenda haki.

Joseph Kasheku (Msukuma) - Mbunge wa Geita vijijini

“Rais mstaafu Bwana Tenga ni mtu wa kuigwa katika kwenye hii tasnia ya michezo, ni Kiongozi ambaye alifanya kazi vizuri na akastaafu na bado wanamtumia lakini ni mtu anayeheshimika kwenye tasnia ya michezo. Sasa wale mliopo kwenye madaraka muige mfano wa jinsi gani Mzee Tenga aliongoza michezo yetu hapa Tanzania”

“Mheshimiwa Mwenyekiti namuuliza kaka yangu Kabudi mheshimiwa waziri, na nilikuona kutokana na mgogoro uliopo kwenye timu zetu hizi kubwa mbili nilikuona ulitoka saa nne usiku kwenye kikao lakini baada ya kutoka mle shaaa, mpaka leo hatujajua kilichotokea kule. Simba na Yanga ndio burudani pekee iliyobaki kwa watu wote, kwanini tuendelee kusikia tu ngojera mitandaoni. Ulichokisikia tueleze, hili ndio bunge la Wananchi.”

“Naamini Simba hawana makosa, Yanga hawana makosa, lakini kinachoendelea nani anayetakiwa kutueleza taarifa sahihi? Kama kesi imekwenda CAS imerudi CAS, imekuja huku kabla mlalamikaji hujamsikiliza unatangaza mechi. Anacheza boli ya Ligi ana cheza Yanga?” - Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma.