Jumanne , 13th Apr , 2021

Golikipa mahiri wa kimataifa wa Uganda Denis Onyango anayechezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini, ametangaza rasmi kustaafu kuchezea timu ya taifa ili kupisha damu changa kuonesha uwezo wao.

Denis Onyango katika moja ya mechi ya Uganda Cranes

Onyango aliyedumu katika timu hiyo ya taifa 'Uganda Cranes' kwa miongo miwili ndani akicheza kwa mafanikio makubwa iliwemo kushiriki AFCON mbili ya mwaka 2017 kule Gabon na 2019 iliyofanyika Misri.

Historia ya nahodha huyu wa zamani wa Uganda Cranes aliyezaliwa 15/5/1985 inaanzia kwenye timu maarufu Uganda na Afrika mashariki na kati Villa SC, ambayo alijiunga nayo akiwa mdogo hatimaye kupandisha kikosi cha kwanza cha wakubwa mwaka 2004, baadaye kutimukia St George ya Ethiopia kabla ya kuingia Africa kusini na kuzichezea timu kadhaa ikiwemo hii ya sasa ya Mamelodi Sundowns.

Onyango mchezaji bora mwaka 2016 kwa wachezaji wa ndani wanaocheza ya bara la Africa, amefanikiwa kutwa ubingwa wa ligi kuu ya Africa kusini mara 7 akiwa na vilabu vya Super Sport 3 na Mamelodi Sundown mara 4

Ameshinda ubingwa wa Africa mwaka 2016 pamoja na CAF super cup,alishiriki pia kombe la Dunia ngazi ya vilabu mwaka 2016, kwa mujibu wa shirika moja linalofanya tafiti za wachezaji mbalimbali duniani lilimuorodhesha kama golikipa bora namba 10 duniani kwa mwaka 2016.

Akiwa katika timu ya taifa ameichezea jumla ya michezo 75 kwa michuamo yote aliyoshiriki, alitajwa kuwa nahodha wa Uganda Crenes mwaka 2017.