Jumanne , 1st Mar , 2022

Mchezaji nyota wa Memphis Grizzlies Ja Morant amevunja rekodi yake aliyoweka siku mbili zilizopita ya kufunga alama nyingi kwenye mchezo mmoja wa NBA baada ya kufunga alama 52 alfajili ya leo kwenye mchezo dhidi ya San Antonio Spurs, mchezo ambao Grizzlies imeshinda kwa 118-105.

Ja Morant mchezaji wa Memphis Grizzlies

Morant amevunja rekodi yake aliyoweka Jumamosi iliyopita ya kufunga alama 46 kwenye mchezo dhidi ya Chicago Bulls ambao walishinda kwa alama 116-110, lakini pia amemaliza mchezo huo akiwa na rebound 7 na pasi za mwisho za kufunga (asisst) 2, akiisaidia Memphis Grizzlies kushinda mchezo wa pili mfululizo.

Na MVP mara mbili wa NBA Giannis Antetokounmpo wa Milwaukee Bucks ameandika rekodi ya kufunga (double doble) kwenye michezo mitano 5 mfululizo baada ya kufunga alama 26 na rebound 16 dhidi ya Charlotte Hornets, mchezo ambao Bucks imeshinda kwa alama 130 kwa 106. Lakini pia Giannis ametoa pasi za kufunga (asisst) 6 na rebound 4.

Giannis Antetokounmpo 

matokeo ya michezo mingine iliyochezwa alfajili ya leo, Sacramento Kings imeifunga Oklahoma City Thunder kwa alama 13 1kwa 110, Chicago Bulls wamefungwa na Miami Heat kwa alama 112 kwa 99, Toronto Raptors wameinyuka Brooklyn Nets kwa 133 kwa 97m Orlando Magic wameifunga Indiana Pacers kwa alama 119 kwa 103 na Minnesota Timberwolves wameshinda kwa alama 127 kwa 122 dhidi ya Cavaliers.