Jumatano , 4th Mei , 2016

Mashirika na watu binafsi wametakiwa kuongeza nguvu katika vituo mbalimbali vya kukuza vipaji vya soka la vijana ili kuweza kupata wachezaji bora zaidi hapo baadaye.

Kocha wa Timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys Bakary Shime amesema, ili vijana wacheze ni lazima kuanza na vijana wadogo kabisa ambao wanatoka katika mashule na taasisi za mitaani ambazo hujitolea hivyo kama nguvu itaongezeka katika maeneo hayo kutakuwa na wachezaji wengi ambao wataweza kuliendeleza soka la Tanzania.

Shime amesema, vituo mbalimbali vinavyoendeleza vijana wanaanza nao lakini baadaye wanashindwa kutokana na kukosa watu wa kuwasaidia kwa ajili ya kuendelea ili kuweza kufanya vizuri zaidi.

Shime amesema, jamii isiangalie Serikali peke yake kuwa itaweza kusaidia vijana au shirikisho la Soka bali wafikiria kwanza kuwa wao kama jamii ndio wanatakiwa kuanza kukuza vijana kabla Serikali haijawaona.