Jumatano , 11th Mei , 2016

Kocha Mkuu wa klabu ya Maji Maji ya mjini Songea, Kally Ongala amesema anafurahia maisha ya mjini Songea tangu aichukue timu hiyo kwenye kipindi cha dirisha dogo.

Ongala amesema wachezaji wa timu hiyo ni wenye kutaka mafanikio, hivyo wanampa morali ya kufundisha kikosi hicho tofauti na alivyofikiria mwanzoni kutokana na kuzoea maisha ya Dar es Salaam.

Ongala aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa klabu ya Azam FC kwa miaka kadhaa, lakini aliicha klabu hiyo na kwenda nje kwa masomo na kisha kurudi nchini mwaka jana na kujiunga na Maji Maji mwishoni mwa mwaka huo huo.