
Patrice Motsepe mgombea pekee wa Urais CAF
Shirikisho hilo la soka Africa ndiyo chombo cha juu cha mchezo huo kwa bara zima, wataingia katika mkutano huo wakiwa na ajenda 25 ikiwemo suala la ripoti za mapato na matumizi ya fedha, japo ajenda inayoonekana kuwavutia wengi ni ile ya uchaguzi hasa kwenye nafasi ya Urais.
CAF kwa sasa ipo chini ya utawala wa rais Ahmad Ahmad aliyeingia madarakani Machi 2017 baada ya kumshinda Issa Hayatou katika uchaguzi uliokuwa na vuta nikuvute kutokana na ukongwe wa Hayatou katika shirikisho hilo aliloliongoza kwa miaka 29 ,
Upepo unaonekana kumuendea vizuri bilionea kutoka Africa kusini Patrice Motsepe mwenye umri wa miaka 57 ambaye ndiyo mgombea pekee kwenye nafasi hiyo, baada ya wagombea kama Augustino Senghor wa Senegal, Jaques Anouma wa Ivory Coast na Ahmad Yahya wa Mauritania kuamua kujitoa na kumuunga mkono.
Motsepe mfanyabiashara mkubwa wa madini anayemiliki migodi kadhaa mikubwa nchini Africa kusini ,ambaye pia ni mmiliki wa klabu ya soka ya Mamelod Sundowns ambayo imekuwa inafanya vizuri katika michuano mbalimbali ya CAF, ameweka bayana sera zake ikiwemo kuitafutia mikataba minono ya haki za matangazo ya Television katika mashindano mbalimbali.
Wakati huohuo, aliyekuwa mgombea wa ujumbe kwenye baraza la shirikisho la soka la kimataifa (FIFA Council) kwa mataifa yanayozungumza kingereza kwa kupitia uchaguzi huu, Wallace Karia ambaye ni Raisi wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) amejitoa katika kinyang'anyiro hicho ili kuweka nguvu katika kutumikia taasisi hiyo.