
Nahodha wa kikosi cha Simba Musa Hassan.
Mgosi amesema wao kama wachezaji wanastahili lawama kwasababu wamechangia maumivu kwa kundi kubwa la mashabiki wao ambao kwa kipindi cha misimu mitatu hawana furaha kutokana na kufanya kwao vibaya.
“Kama wachezaji tunastaili kubeba lawama za mwenendo mbaya wa timu na hata kuuliwa kwasababu hatukuweza kutimiza majukumu yetu ipasavyo na wengi wetu hatujui historia ya timu hii na upinzani uliopo kati ya Simba na Yanga,” amesema Mgosi ambeye tangu amerejea Simba msimu huu hajafunga hata bao moja.
Aidha, nahodha huyo alisisitiza kuwa kwa mtu mwenye akili timamu na anayejua Simba inataka nini, lazima aumie.