Jumamosi , 5th Jul , 2014

Kamati ya usajili ya klabu ya Simba kufanya kikao kizito cha kujadili mapendekezo ya kocha Logarusic watatoa maamuzi ya mwisho ya juu ya nani anasajiliwa na nani anaachwa katika kikosi cha msimu ujao wa ligi kuu bara VPL

Kocha mkuu wa Simba Zdravko Logarusic ambaye atawasili wiki ijayo akitokea nchini kwao Croatia alikokua mapumzikoni.

Kamati ya usajili ya klabu ya soka ya Simba inataraji kukutana kesho kwaajili ya kikao cha tathmini na kupitia mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo mcroatia Dzavko Logarusic ambaye anataraji kuwasili nchini wiki ijayo.

Afisa habari wa klabu hiyo Asha Muhaji amesema kumekua na taarifa nyingi kuhusu usajili wa klabu hiyo lakini ukweli wa yote utajulikana siku chache zijazo baada ya kikao hicho cha kesho cha kamati ya usajili ya klabu hiyo iliyo chini ya mwenyekiti Zakaria Hans Pope na katibu wake Khasim Dewji

Aidha Muhaji amesema timu hiyo inataraji kuanza mazoezi ya "Off Camp" wiki ijayo na baadae ikishakamilisha zoezi la usajili ndio itakwenda nje ya nchi kwaajili ya kambi ya maandalizi ya ligi kuu msimu ujao utakao anza August 23 mwaka huu.