Kamusoko na Rostand waachwa

Jumatano , 14th Feb , 2018

Kocha George Lwandamina wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga, ameendelea kuwaweka nje ya kikosi kiungo Thabaani Kamusoko na mlinda mlango Youthe Rostand licha ya kuelezwa kuwa wamepona.

Nyota hao hawajajumuishwa kwenye kikosi cha leo kinachocheza mchezo wa ligi kuu raundi ya 18 dhidi ya Majimaji FC licha ya jana daktari wa timu hiyo Dr. Bavu kuweka wazi kuwa wamepona.

Kwa upande wa golini kocha Lwandamina ameendelea kumwamini chipukizi Ramadhani Kabwili ambaye atakuwa anadaka mechi yake ya tatu mfululizo akianza ikiwemo ile ya Ligi ya mabingwa Afrika jumamosi iliyopita dhidi ya St. Louis.

Yanga imekuwa na matokeo mazuri katika mechi zake za hivi karibuni ambapo imeibuka na ushindi wa kwenye mechi zake tano wakianza na 0-1 dhidi ya Ruvu Shooting  2-1 dhidi ya Azam, Lipuli 0-2 Yanga na Yanga 4-0 dhidi ya Njombe Mji kabla ya kushinda 1-0 mchezo wa kimataifa dhidi ya Yanga

Kikosi kamili cha leo
1. Kabwili 2. Kessy 3. Gadiel 4. Makapu 5. Chikupe 6. Maka 7. Buswita 8. Tshishimbi 9. Chirwa 10. Ajib 11. Martin
Wachezaji wa akiba: Beno, Abdul, Nadir, Daud, Mahadhi, Haji, Mwashiuya.