Jumamosi , 11th Dec , 2021

Mapacha wa Kariakoo, vilabu vya Simba na Yanga vinataraji kuchezwa saa 11:00 Jioni ya leo Disemba 11, 2021 kwenye dimba la Mkapa ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa 8 wa Ligi kuu NBC Tanzania.

(Simba na Yanga zilipokutana Septemba 25, 2021 Fainali ya Ngao ya Jamii)

Kuelekea kwenye mchezo huo, tayari rekodi za misimu minne  zinaonesha kuwa wawili hao wametoshana nguvu katika michezo minne, Simba ikishinda michezo miwili na Yanga ikishinda michezo miwili.

Mshindi wa mchezo huo basi ataruka kihunzi cha kutoshana nguvu na badala yake atakuwa ameibuka na ushindi wa uongozi na watambo ndani ya miaka hii minne kwenyemichezo ya Ligi kuu pekee.

Mbali na rekodi hiyo, wawili hao walikutana mara ya mwisho kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Hisani ya Jaimii Septemba 25, 2021 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 1-0 bao lililofungwa na Fiston Mayele.

Simba huenda itamkosa Taddeo Lwanga ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni wakati Yanga itaendelea kumkosa Yacouba Songne ambaye anauguzu majeraha yake ya goti baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Tunisia.

Wawili hao wamekutana mara 106, Yanga ikipata ushindi kmara 38, Simba mara 31 na kutoa sare 37.