
Mtendaji Mkuu wa Azam Fc Abdulkarim Amin (kushoto) akiwa na Kocha wa kikosi hicho Abdi Hamid Moallin katika picha ya pamoja
Popat ameyasema hayo akiwa anaweka wazi juu ya malengo yao waliyonayo msimu huu ambapo amesema wanaendelea kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara licha ya baadhi ya wadau wakiwa hawana imani nao kwakuwa ni muda mrefu tangu watwae ubingwa huo tangu wafanye hivyo msimu wa 2013/14.
''Malengo yetu ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, na hilo halijabadilika, ni kweli hatujachukua kwa muda mrefu lakini kama mnavyofahamu Simba na Yanga ndio timu zilizojizatiti kwa muda mrefu hivyo si rahisi kuziangusha lakini tupo kwenye njia sahihi ya mafanikio na tutafanikisha hilo''alisema Popat.
Azam ilianza kwa kusuwasuwa msimu huu hali iliyosababisha wamfute kazi Kocha wao Mkuu, George Lwandamina na nafasi yake imechukuliwa na Abdi Hamid Moallin ambaye amebadili taswira ya timu hiyo na sasa inapata matokeo mazuri uwanjani.
Hadi sasa Azam wanakamata nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na alama 21 zikiwa ni 4 nyuma ya mabingwa watetezi Simba wenye alama 25, na alama 14 nyuma ya Yanga ambao ndio vinara wakiwa na alama 35.