Ijumaa , 9th Apr , 2021

Mwamuzi Jesus Gil Manzano ameteuliwa kuwa mwamuzi wa pambano kubwa la ligi ya Uhispania maarufu kama La liga katika mchezo utakaochezwa jumamosi hii ya tarehe 10/4/2021.

Jesus Gil Manzino mwamuzi atakaye chezesha El Clasico

Gil Manzano anachukua nafasi ya Antoin Mateo Lahoz ambaye alikuwa chaguo la kwanza la kamati ya waamuzi wa la Liga (CACP), bahati mbaya aliumia katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich dhidi ya PSG uliomalizika kwa wenyeji kupoteza 3-2.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Gil Manzino kuchezesha El Clasico, kwani kwa mara ya kwanza alichezesha msimu wa 2014/15 ambapo Real Madrid waliibuka na ushindi wa 3-1 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mwamuzi huyu amezichezesha timu zote mbili jumla ya michezo 51 na wapinzani tofauti,ambapo kwa upande Real Madrid amechezesha michezo 31 ameshinda 25, amesare 3 amepoteza 3 pia, kwa upande wa Barcelona amechezesha michezo 20, wameshinda 11 wamesare 5 na wamepoteza 4.

Katika msimu huu amechezesha mchezo moja wa Barcelona dhidi ya Real Sociedad iliyomalizika kwa sare 1-1, huku akiwa na rekodi binafsi ya kuwa moja ya waamuzi wachache kuwahi kumpa kadi nyekundu Lionel Messi.