Jumapili , 13th Oct , 2019

Kinda wa klabu ya Simba, Joseph Peter ambaye amecheza kwa mara ya kwanza jana katika timu ya wakubwa amefichua siri kubwa iliyomsaidia kuwa na kiwango kizuri uwnjani.

Kinda Joseph Peter na Pascal Wawa

Mchezaji huyo ambaye ametoka katika timu ya vijana ya Simba na kucheza jana kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Bandari amesema kuwa kitu ambacho kilimsaidia kutulia uwanjani ni ushauri ambao alipewa na mlinzi mkongwe Pascal Wawa.

"Pascal Wawa alikuwa ananiambia nitulie nisiforce sana kupanda juu kwa sababu Bandari wananizidi kuanzia nguvu na spidi, kwahiyo na mimi nikawa najitahidi kufanya vile ambavyo nilikuwa naagizwa", amesema Joseph.

Aidha Joseph Peter amemtaja mlinzi Mohamed Hussein 'Tshabalala' kuwa ndiye mchezaji anayemkubali katika kikosi cha Simba na kwamba ana mipango mikubwa katika soka kwani yupo katika klabu ya Simba kama njia ya kuyafikia mafanikio hayo.