
Neymar akiwa tumbo wazi huku ameshikilia jezi mkononi aliyobadilishana na mchezaji wa Rb leipzig Marcel Halstenberg baada ya mchezo kati ya PSG na RB Leipzig kumalizika.
Psg ilifuzu fainali ya ligi ya mabigwa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo tangu iliyoanzishwa mwaka 1970 baada ya kuifunga timu ya Rb Leipzig ya Germany kwa bao 3-0 na hivyo kumsubiri mshindi kati ya Lyon na Bayern Munich zitakazoumana usiku wa leo.
Baada ya mchezo huo kuisha nyota wa timu hiyo Neymar alibadilishana jezi na mchezaji wa Rb leipzig Marcel Halstenberg kama tamaduni za soka kabla ya janga la Corona, kwa kitendo hicho Neymar anatafsirika kukiuka kanuni za kuthibiti janga la COVID-19 ambapo adhabu ni kukosa mchezo moja.
JE PSG ITAATHIRIKA VIPI IWAPO ITAMKOSA NEYMAR?
Kiufundi endapo Psg watamkosa Neymar katika mchezo wa fainali itawaathiri sana timu hiyo ambayo inacheza kwa ushirikiano mkubwa wa wachezaji watatu kwenye safu ya ushambuliaji ambaye ni Neymar Kylian Mbappe na Angel di Maria.
Hivyo wapinzani wanaweza wasiwe na uoga tena na kujipanga vizuri kuwathibiti wachezaji waliobaki kiwepesi ukifananisha na siku anazokuwepo Neymar ambayo katika hatua hizi anaonekana kuwa katika kiwango bora cha kiuchezaji.
JE PENGO LA NEYMAR LINAZIBIKA?
Si rahisi kuziba pengo la Neymar Jr kutokana na aina ya wachezaji waliopo mfano Choupo Moting, Pablo Sarabia na Mauro Icardi, kwa hawa aina yao ya uchezaji ni tofauti na mbrazil huyo.
Hivyo kama Kocha Mjerumani Thomas Tuchel atataka kupata ushindi atalazimika kubadili mbinu zake za kucheza pasipo kufiria kuziba pengo la Neymar ambaye ana kipaji cha kipekee ukilinganisha na hao waliotajwa.