Kikosi cha KMC FC
Wachezaji wa KMC watakao ukosa mchezo wa kesho ni Golikipa Farok Shikalo ambaye alipata majeraha kwenye mazoezi, na Kelvin Kijiri ambaye aliumika katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na Miraji Athumani atakekosekana kwa mambo ya kifamilia.
Kwenye rekodi Polisi Tanzania haijawahi kufungwa na KMC kwenye michezo 5 waliokkutana Polisi wameshinda michezo yote, ikiwemo mchezo wa mkondo wa kwanza msimu huu ambao KMC walinyukwa mabao 2-0.
Licha ya rekodi kutokuwa nzuri upande wao dhidi ya Polisi lakini Msemaji wa KMC Cristina Mwagala ameahidi kuvunja mwiko huo kwa kushinda mchezo wa kesho.
“ Tunakwenda kucheza na Polisi ni Timu nzuri, lakini KMC ni bora sana, pamoja na kuwa hatujawahi kuwa na matokeo rafiki pindi tunapokutana lakini awamu hii tutahakikisha tunashinda mchezo wetu, wachezaji wetu wote wapo vizuri ,wana hali nzuri na morali nzuri pia, kwa hiyo kikubwa tuombe uzima wachezaji wote wa amkesalama.” Amesema Mwagala
Timu hizi pia zina alama sawa kwenye msimamo wa Ligi zote zina alama 19 katika michezo 15, Polisi wapo juu kutokana na faida ya magoli ya kufunga na kufungwa wapo nafasi ya 8 na KMC FC wapo nafasi ya 9.


