KMC wasema sio Azam FC pekee

Alhamisi , 6th Dec , 2018

Kuelekea pambano la ligi kuu soka Tanzania bara, kati ya timu mbili za Dar es salaam, KMC na Azam FC, Jumatatu ijayo, KMC wamesema wapinzani wao sio Azam FC pekee kama ambavyo imekuwa ikionekana wakati wa mechi yao.

Wachezaji wa KMC kushoto na Azam FC kulia.

Akiongea leo na www.eatv.tv  kocha msaidizi wa KMC Ahmed Ally, amesema maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam FC ni kama mchezo mingine tofauti na watu wanavyodhani kuwa mchezo huu tunaupa umuhimu kuliko mechi zingine.

''Upinzani wetu na Azam FC ni kama tu wa Mwadui FC maana kila mchezo kwenye ligi sisi tunauchukulia kwa uzito uleule ila kwasababu sisi ni timu ya mjini hapa na Azam FC ni hapa pia inaonekana kama tuna ushindani wa pekee'', amesema.

KMC ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 17 kwenye michezo 14, wakati Azam FC inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 36 kwenye michezo 14. Pia hawajapoteza mchezo hata mmoja wa ligi msimu huu.