Ijumaa , 21st Dec , 2018

Klabu ya soka ya KMC imeanza vyema kampeni ya kuipata tiketi ya kushiriki michuano ya shirikisho barani Afrika, baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa Azam Sports Federation Cup (AFC) dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo wa KMC dhidi ya Tanzania Prisons

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Uhuru, umeshuhudia dakika 90 zikikamilika kwa sare tasa na kupelekea hadi katika hatua ya mikwaju ya penati ambapo wana 'Kino Boys' wameibuka na ushindi wa penati 4-3.

Baada ya matokeo hayo, sasa KMC inasonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo mshindi wake hupata tiketi ya kushiriki michuano ya shirikisho barani Afrika.

Katika matokeo mengine, Ruvu Shooting ya Afisa Habari mwenye majigambo, Masau Bwire imeshuhudia ikishangazwa katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kutupwa nje kwa mikwaju ya penati 5-6 dhidi ya Mighty Elephant .

Matokeo ya jumla ya michezo ya leo ni:

KMC  0-0  Tanzania Prisons (Pen 4-3)
Changanyikeni  1-4  Coastal Union
Ruvu Shooting  1-1  Mighty Elephant
Mufindi United  0-3  Alliance FC
La Familia  1-0  Mawenzi  Market