Jumanne , 31st Mar , 2015

Kocha wa Timu ya Tanzania Prisons, Mbwana Makata amesema, anaamini kikosi chake hakitaweza kushuka Daraja kwani ligi bado haijafika mwisho kwa msimu huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Makata amesema licha ya timu hiyo kuwa katika nafasi ya mwisho huku ikiwa na Pointi 17 katika msimamo wa ligi kuu Soka Tanzania Bara anaamini mazoezi pamoja na ushirikiano wa wachezaji wawapo uwanjani utasaidia kwa kiasi kikubwa timu kuwa katika nafasi nzuri.

Makata amesema, ameanza kuifundisha timu hiyo katikati mwa Ligi, lakini amefanikiwa kuyafanyia kazi mapungufu aliyoyakuta kwa wachezaji na ameboresha kikosi hicho ambacho ana imani kitaweza kufanya vizuri katika mechi zilizobakia.