Kocha Stars ataja siri ya kuifunga Burundi

Jumapili , 8th Sep , 2019

Kocha wa timu ya Taifa Tanzania, Etienne Ndayiragije, amesema wataibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo, dhidi ya Burundi, kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika 2022, Qatar.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake Kocha Ndairagije, amesema wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele.

Amesema kazi kubwa ya kumaliza mchezo huo waliifanya tangu walipokuwa ugenini ambapo walitoka sare ya kufungana bao kwa moja.

"Mchezo wa marudiano utakuwa wa kufa au kupona kwa sababu ndiyo utakaamua mustakabali wetu, lazima tutumie vema uwanja wetu wa nyumbani kupata matokeo mazuri na kusonga mbele." amesema Ndayiragije

Kwenye mchezo wa leo Stars inahitaji kusonga hadi hatua ya makundi, ebdapo itatoka sare ya aina bila kufungana au ushindi, huku wapinzani wao Burundi wakihitaji ushindi pekee ili kupiga hatua nyingine mbele.