Kocha wa Yanga ailalamikia Mbeya City

Jumatano , 12th Feb , 2020

Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa sababu iliyopeleka kushindwa kupata pointi tatu dhidi ya Mbeya City ni kutokana na aina ya mchezo waliocheza wapinzani wao.

Kocha wa Yanga, Luc Eymael

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa na kulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Mbeya City ikipata bao katika kipindi cha kwanza na Yanga ikisawazisha kipindi cha pili.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Luc Eymael amesema, "sisi tumecheza vizuri lakini unaona wapinzani wetu walivyocheza, walikuwa wamejaa nyuma na kubakiza mchezaji mmoja mbele".

"Makosa yalifanyika katika kipindi cha kwanza na kupelekea bao tulilojifunga, lakini tulikuwa bora zaidi kipindi cha pili na tukapata bao lakini shida bado ilikuwa namna walivyokuwa wakicheza nyuma", ameongeza.

Mbeya City ipo katika hatari ya kushuka daraja, ikiwa katika nafasi ya 19 na pointi 18 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 38 baada ya kucheza mechi 19.