Jumatano , 7th Mei , 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kitendo cha Urusi kushiriki Kombe la Dunia 2026 kinaweza kuwa motisha na fursa  ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Rais wa Marekani Donald Trump

Hayo ameyasema  katika mkutano wa kwanza wa kikosi kazi cha utawala wake katika kikao cha maandalizi ya kombe la Dunia la 2026 ambapo  Trump amesema kuirejesha Urusi katika mashindano hayo kunaweza kumaliza vita nchini Ukraine.

Ikumbukwe kwa mujibu wa sheria za sasa Urusi haitacheza kombe la Dunia la 2026 linaloandaliwa  na Marekani, Canada na Mexico baada FIFA na UEFA kulipiga marufuku  taifa hilo kushiriki mashindano ya kimataifa tangu nchi hiyo ilipoivamia Ukraine mwaka 2022.

“Tunataka hii vita imalizike haiwezekani watu wanapoteza maisha kila kukicha wakati tunayo njia ya kufanya mazungumzo na kuyamaliza” Trump akiwa ameketi karibu na rais wa FIFA Gianni Infantino, Trump hakujua kuwa Urusi ilipigwa marufuku kushiriki michuano hiyo.