Kukosekana kwa Samatta, Msuva aeleza madhara

Alhamisi , 10th Oct , 2019

Winga wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza katika klabu ya Difaâ Hassani El Jadidi ya Morocco, Simon Msuva amesema, kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda wanategemea mwalimu atawapanga vizuri kufuatia kutokuwepo kwa nahodha Mbwana Samatta.

Msuva, Samatta na wachezaji wengine katika moja ya mechi za taifa Stars

'Sisi kama wachezaji tunaheshimu uwepo wa nahodha Mbwana, ila kutokuwepo kwake kama wachezaji lazima kuna pengo tutaliona ila tunaamini mwalimu ameshaliona hilo na kwasababu tupo wachezaji wengi wa mbele atatupanga vizuri'.

Kuhusu yeye na muunganiko wake na Samatta anapokuwepo uwanjani, Msuva amekiri kuwa Samatta kama nahodha anakuwa na kitu cha tofauti na huwa ana wapa nguvu uwanjani ila watajitahidi kuhakikisha wanafanya kila njia ili kushinda.

Kwa mujibu wa taatifa kutoka katika kambi ya taifa Stars, Samatta ameomba kupata muda wa kupumzika kwa kile kilichoelezwa anaendelea kupona kutoka kwenye majeraha madogo aliyopata.

Tanzania itacheza na Rwanda ugenini Jumatatu, Oktoba 14, 2019. Mchezo huo ni wa kirafiki unaotambulika na kalenda ya FIFA.