Jumatano , 31st Mar , 2021

Mabingwa wa ulaya klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imejitoa kwenye mbio za kumuwania mshambuliaji Erling Haaland wa Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu kwa sababu tayari wanamshambuliaji bora Dunia Robert Lewandowski, amesema mtendaji mkuu wa klabu hiyo Karl-Heinz Rummenigge.

Robert Lewandowski kushoto na Haaland kulia

Haaland mwenye umri wa miaka 20, amekuwa akihusisha kujiunga na vilabu kadhaa barani ulaya ikiwemo Bayern Munich, Real Madrid, FC Barcelona, Chelsea, Manchester United na Manchester City, hii ni kutokana na kiwango bora alichoonyesha mshambuliaji huyo.

Karl-Heinz Rummenigge akijibu kuhusu Bayern Munich kuwa ni moja ya timu inayotajwa kuwa kwenye mbio za kumsajili kinda huyo mwishoni mwa msimu huu amesema,

“Sijui uvumi huo unatoka wapi. Ninaweza kusema jambo moja tu, tunamchezaji bora kwenye hiyo nafasi, Robert Lewandowski anamkataba hadi mwaka 2023, kama nilivyosema mchezaji huyo bora Dunia anakaribia kuifikia rekodi ya Gerd Muller ya kufunga mabao 40 ndani ya msimu mmoja kwenye Bundesliga, na kwa sasa yupo kwenye kiwango bora cha maisha yake”.

Haaland amefunga mabao 25 kwenye ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga msimu huu na amezidiwa mabao 10 na Lewandowski ambao ndio kinara wa ufunngaji akiwa na mabao 35, na imesalia michezo 8 kabla ya msimu kumalizika.