Jumanne , 18th Aug , 2020

Romelu Lukaku ni mshambuliaji ambaye alijiunga na Inter Milan akitokea Manchester United msimu juzi, na sasa amekua tegemeo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na muitalioano Antonio Conte,msimu huu kafunga jumla ya mabao 33 kwenye mashindano yote, huku akiweka rekodi mbalimbali.

Mshambuliaji wa Klabu ya Inter Nilan, Romelu Lukaku akishangilia baada ya kufunga bao katika Serie A.

EATV inakusogezea rekodi mbali mbali za nyota huyo alizoziweka na anazotarajiwa kuziweka mara baada ya msimu kumalizika.

Mosi,alikua mchezaji wa kwanza wa Inter Milan Kufunga bao 9 katika mechi 11 za kwanza za Serie A tangu ajiunge na Klabu hiyo.

Kwa mara ya mwisho mchezaji wa Nerazzurri kufanya hivyo ilikua katika msimu wa 1997/98 kupitia Ronaldo Nazario de Lima.

Pili, Lukaku alikua mchezaji wa kwanza wa Inter kufikisha bao 30 na zaidi ndani ya msimu mmoja, tangu Samuel Etoo afanye hivyo msimu wa 2010/11 ambapo alifikisha bao 37 katika mashindano yote.

Tatu,Lukaku alikua mchezaji wa kwanza wa Nerazzurri kufikia rekodi iliyodumu kwa miaka 70 ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 15 katika viwanja vya ugenini katika Serie A ndani ya msimu mmoja,rekodi hiyo iliwekwa na Stefano Nyers mwaka 1950.

Nne,Nyota huyo alimaliza msimu wa Serie A akiwa wa tatu kwenye orodha ya wafungaji bora nyuma ya kinara Ciro Immobile (36), Cristiano Ronaldo (31) wakati Lukaku alikua na bao (23) akiwapiku Diego Milito na Amedeo na Amadei katika msimu wao wa kwanza ndani ya Inter.

Tano, Lukaku  pia aliweka rekodi yake binafsi ya kufunga mabao mengi katika msimu mmoja, bao 30, kwa mara ya mwisho kufunga idadi ya mabao mengi ndani ya msimu  alikua na Man United msimu wa 2017/18 ambapo alifikisha mabao 27 katika mashindano yote.

ALICHOKIKOSA

-Alibakisha bao 1 kufikia rekodi ya Ronaldo de Lima ambaye katika msimu wake wa Kwanza na Inter alimaliza na bao 23.

KIPI ANAWEZA KUKIFIKIA?

-Hadi sasa Romelu Lukaku amefunga jumla ya mabao 33 katika mashindano yote msimu huu.

-Iwapo atafunga katika Fainali ya Europa League dhidi ya Sevilla, ataifikia Rekodi ya Ronaldo Nazario De Lima ambaye katika msimu wake wa kwanza na Inter wa 1997/98 alimaliza msimu na bao 34.

AKIWA NA MAN UTD

2018/19-Bao 15

AKIWA NA INTER

2019/20-Bao 33