
Katibu wa Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania TAHA Kaushik Ndoshi amesema kwa upande wa timu ya wanawake licha ya kushinda mechi yao ya juzi dhidi ya Botswana kwa mabao 3-0 lakini imeshindwa kusonga mbele kutokana na kupoteza mechi zake za awali.
Doshi amesema, kwa upande wa wanaume walipoteza mechi zao ,nili mfululizo dhidi ya wenyeji Namibia kwa mabao 23-0 na Egypt kwa mabao 28-0.
Timu hizo ambazo zimepoteza nafasi ya kucheza fainali za dunia za mchezo huo kwa vijana baada ya kupata matokeo mabovu zinatarajiwa kurejea Jumatatu ya Machi 28 mwaka huu.
Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi Machi 18 mwaka huu ambapo yatafikia tamati Machi 28 na yameshirikisha nchi zote wanachama wa mchezo huo Barani Afrika.