Kocha wa Maji Maji, Habib Kondo amewataja wachezaji waliosimamishwa ni Andrew Ntala, Sadik Galacha, Paul Maona, Alex Kondo na Six Mwasegaga.
Kondo ameweka wazi kuwa wachezaji wote hao wamesimamishwa kwa kosa la kugoma kufanya mazoezi, huku pia wakiwachochea wachezaji wengine kufanya hivyo.
Kwa upande wa taarifa kutoka kwa wachezaji zinaeleza kuwa waligoma ili kushinikiza kulipwa stahiki zao mbalimbali, ikiwemo malimbikizo ya mishahara, fedha za usajili pamoja na posho.
Aidha Kondo ameongeza kuwa amechukua wachezaji kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwajili ya kuziba nafasi hizo. Mchezo huo wa leo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni.





