Ijumaa , 20th Feb , 2026

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kuuza tiketi zote zilizotolewa kwa ajili ya mchezo wa fainali wa Kombe la Carabao dhidi ya Arsenal, utakaofanyika kwenye Uwanja wa Wembley Machi 22.

Earling Haaland

Manchester City ilipata mgao wa tiketi 31,939 pamoja na viti vinavyoweza kufikiwa kwa urahisi kwa watu wenye uhitaji maalum.

Mauzo ya tiketi za klabu hiyo yanaonyesha hamasa kubwa ya mashabiki kuelekea mchezo huo muhimu.

Hadi sasa Arsenal ambayo itacheza fainali na Man City haijatoa ripoti maalum ya mauizi ya tiketi zao.