Jumapili , 1st Mei , 2016

Leicester lazima isubiri mechi mbili zilizobaki, kutwaa taji la ligi kuu ya soka nchini Uingereza, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford jioni ya leo.

Leicester lazima isubiri kutwaa taji la ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford jioni ya leo.
 
Wakihitaji ushidi huo wa kihistoria katika kipindi cha miaka 132,vijana wa kocha Claudio Ranieri walionyesha kuwa na wasi wasi na baada ya dakika ya 8, United kutikisa wavu wa Mbweha hao, kwa bao la Anthony Martial.
 
Lakini wageni hao walitulia na kuonyesha kuwa ndiyo vinara wa ligi hiyo, na kupata bao la kusawazisha la nahodha wao Wes Morgan dakika tisa baadae.

Wakati huo huo, Liverpool imeangukia pua baada ya kunyukwa mabao 3-1 na Swansea City.