
Haji Manara na mtoto shabiki wa Simba
Katika ukurasa wake wa Instagram, Manara ameweka video ya mtoto huyo akiambatanisha na ujumbe unaosema kuwa kwa mwenye taarifa za mtoto huyo awasiliane naye.
Pia jana, Machi 7, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo' alimzungumzia mtoto huyo kuwa ni shabiki halisi wa Simba na anapenda kuona kizazi kijacho kikiendelea kuipenda klabu hiyo.
Kikosi cha Simba kipo nchini Algeria kwaajili ya kupamabana na JS Saoura katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi wa Klabu Bingwa Afrika.