Jumatatu , 20th Apr , 2020

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amezungumzia juu ya kitu kikubwa ambacho kinakosekana kwa mashabiki wa klabu hiyo hivi sasa.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara

Kutokana na ligi kusimama hivi sasa kutokana na janga la virusi vya Corona, Haji Manara amesema kuwa kitu kikubwa ambacho mashabiki wanakikosa hivi sasa ni furaha ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.

Manara amesema kuwa kukosekana kwa uhondo huo kunawapa mawazo kidogo ila kwa kuwa ni kwa ajili ya afya hakuna namna lazima iwe hivyo, "unajua tayari kikosi cha Simba kilikuwa kwenye ubora wake na kwenye mechi zetu mbili za nyuma kabla ya ligi kusimamishwa tulishinda hivyo unaona hapo kulikuwa na ari na morali kiasi gani".

"Kwa sasa ambacho tunakikosa ni mechi pamoja na shangwe la wana Simba kushangilia ushindi wao, kikubwa na muhimu kwa sasa ni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kuwa salama kwani afya ni muhimu," ameongeza.

Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Machi 17,  Simba ilikuwa nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni 71.