Jumatano , 24th Feb , 2016

Kocha wa kituo cha kukuza vipaji vya magoli kipa Peter Manyika amesema, ameamua kumrudisha kijana ambaye alikuwa katika majaribio nchini Msumbiji kwa ajili ya kutokuafikiana makubaliano kati yake na viongoizi wa timu ya polisi mji wa Nampula.

Manyika amesema, katika majaribio walitakiwa kuondoka wawili lakini mmoja ambaye ni Said Kipao alishindwa kutokana na matatizo ya pasipoti.

Manyika amesema, Daudi alikubaliwa lakini wakahitaji kumbadilisha uraia ili kuichezea timu hiyo na baadaye timu ya Taifa.

Manyika amesema, hawakukubaliana na suala la kumbadili uraia mlinda Mlango huyo na wakakubaliana arudi nchini ili kuweza kuendelea na mazoezi mpoaka pale watakapopata timu nyingine.