Alhamisi , 25th Dec , 2014

Kocha wa Magoli kipa wa kituo cha kukuza magoli kipa nchini, Peter Manyika amewataka magolikipa mbalimbali nchini kuendeleza vipaji vyao kwa kuendelea na mazoezi pindi wanapokuwa mapumziko.

Manyika Peter

Akizungumza na East Africa Radio, Manyika amesema katika kituo chake anafundisha magoli kipa kutoka timu mbalimbali za Ligi kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la pili na wengine hawana timu kabisa.

Manyika amesema kwa magoli kipa ambao hawana timu ni wale ambao ndio wameanza hivyo kadri wanavyoendelea na mazoezi katika kituo hicho, kuna timu ambazo huhitaji magoli kipa na wanapokuja kituoni hapo huwachukua kwa ajili yta kusaidia timu zao.

Manyika amesema, magoli kipa hao hufundisha kwa mfumo wa kisasa kutokana na mabadiliko ya mpira wa hapa nchini, Afrika na Duniani kwa ujumla hivyo anaamini magoli kipa hao huwa na masaada mkubwa katika timu ambazo wanakwenda kuzisaidia.

Ameongeza kuwa, kwa magoli kipa wenye timu zinazoshiriki ligi kuu huwa wanaangalia na ratiba na kama wanamechi za mikoani huwa hawafiki kituoni hapo kwa ajili ya mazoezi hivyo mazoezi huendelea kwa wale ambao wapo na kama wanakuwa na mechi za ndani huwa wanapata muda wa kuendelea na mazoezi kituoni hapo pindi timu zinapokuwa kambini.

Manyika amesema mpaka sasa ana magolikipa takribani 21 ambapo anategemea kuwa na magolikipa wengi zaidi kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao kwa faida ya soka la Tanzania.