Jumapili , 5th Jun , 2022

Mastaa wa ndani ya kikosi cha Yanga, wapo kwenye hesabu za kufyekwa kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2022/23.

Nyota wa Yanga Heritier Makambo na Fiston Mayele.

Msemaji wa Yanga, Haji Manara, amesema kuwa usajili wa msimu ujao utakuwa ni mkubwa na wenye kuzingatia ripoti ya benchi la ufundi.

“Tuna malengo makubwa na tunajua wapi ambapo tulishindwa msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa tutasajili wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa ili kuleta ushindani kimataifa,” amesema  Manara.

Habari zinaeleza kuwa, miongoni mwa wachezaji ambao wataachwa moja kwa moja na wengine kutolewa kwa mkopo ni Erick Johore na Ramadhan Kabwili, hawa ni makipa hawajacheza hata mechi moja ya ligi msimu huu.

David Bryson, amecheza mechi 6, Abdallah Shaibu (mechi 1), Deus Kaseke (mechi 10) na Heritier Makambo (mechi 18), Yusuph Athuman (mechi 6), Yassin Mustapha (mechi 9), Paul Godfrey (mechi 1), Crispin Ngushi (mechi 3), Dennis Nkane (mechi 10), Balama Mapinduzi (mechi 1), Chico Ushindi (mechi 5) na Ibrahim Abdallah (mechi 2).