Jumamosi , 5th Oct , 2019

Katika vitu ambavyo vilikuwa vya kusisimu katika fainali ya kwanza ni namna mastaa, Baraka Sadick wa Mchenga na Baraka Mopele wa Tamaduni, walivyochuana kuzipambania timu zao.

Msanii Madee akiwa kwenye uwanja wa Don Bosco ilipopigwa game 1 ya fainali za Sprite Bball Kings

Siku ya Oktoba 4 kulifanyika fainali ya kwanza kati ya tano za mashindano ya Sprite Bball Kings 2019, iliyowakutanisha mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars dhidi ya Tamaduni katika viwanja vya Don Bosco, Osterbay.

Game 1 hiyo ilimalizika kwa timu ya Mchenga Bball Stars kushinda vikapu 122 dhidi ya 121 ya timu Tamaduni.

Aidha kwa upande wa  burudani ya muziki ilihudhuriwa na wasanii kama Madee, Country Boy, Moni Centrozone, Amber Lulu, Official Baila, Duma ,Wakazi, Foby ,Maarifa, Gazza, Rasco Sembo, Domo Kaya, Bonge La Nyau, Ice Boy na 'Producer' Mr T-Touch.

Baada ya mchezo huo kumalizika tulipiga stori na Madee ambaye amesema,

"Mimi nilikuwa nauchukulia poa huu mchezo, sikutegemea kuona mashabiki wengi kiasi hiki, "Vibe" la kutosha, mchezo unatumia nguvu kubwa sana na spidi kuliko hata mpira wa miguu halafu watu walivyokuwa wananihadithia imekuwa tofauti nilivyoona leo, wanasemaga huu mchezo ni wa mabishoo ila sio hivyo ila mtegemee kuniona kuja kuangalia mashindano haya, zaidi na zaidi" ameeleza.

Aidha wakati wa Moni Centrozone na Country Boy wanafanya show waligawana upande wa kushabikia timu hizo ambapo Moni alikuwa Tamaduni na Country Boy alikuwa Mchenga.

Fainali hizo zitaendelea siku ya kesho Jumapili katika uwanja wa ndani wa Taifa kuanzia saa 10 jioni.