Matic bado yupo sana Man United

Jumatatu , 6th Jul , 2020

Nemanja Matic amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia Manchester United

Kiungo wa Manchester United,Nemanja Matic(pichani)katika moja ya mchezo wa ligi kuu ya England.

Kiungo wa klabu ya Manchester United,Nemanja Matic amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2023.

Mkataba wasa sasa wa raia huyo wa Serbia unamalizika mwezi januari mwakani na iliaminika kwamba huenda nyota huyo angeondoka klabuni hapo.

Matic mwenye umei wa miaka31 alijiunga na United mwaka 2017 akitokea Chelsea ambayo aliitumikia kwa miaka mitatu na nusu.

Tangu ajiunge na miamba hiyo ya jiji la Manchester,Matic ameichezea katika mechi 114 na kuifungia mabao manne katika mashindano yote.

Akizungumzia kuhusu mkataba wake mpya,Matic amesema ni faraja kwake kuendelea kuaminika katika klabu hiyo na ataendelea kujitoa kwa nguvu na maarifa ili kuisaidia klabu kufikia malengo yaliyopangwa.

Nae kocha mkuu wa Man United,Ole Gunner Solkjear amesema Matic ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na mzoefu hivyo uwepo wake kwa miaka mingi zaidi,kutaongeza uongozi kwa chipukizi wanaopandishwa katika kikosi chake na kuwapa ari ya ushindi.

Matic amecheza katika mechi tatu mfululizo za Man United ambazo zimewapa ushindi na sasa klabu hiyo inakaribia kufikia malengo ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika ligi kuu ya England.