Jumatatu , 17th Dec , 2018

Draw ya hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya imefanyika leo nchini Uswisi na kushuhudia timu tatu za Uingereza zikipangwa na timu za Ujerumani.

Kombe la Klabu Bingwa Ulaya (kushoto) na Europa League (kulia)

Katika droo hiyo, imeshuhudiwa vigogo wa Bundesliga Bayern Munich ikipangwa na Liverpool ambapo Bayern itaanzia ugenini, mabingwa watetezi wa EPL Manchester City ikipangwa kuanzia ugenini dhidi ya Schalke 04 huku Burussia Dortmund pia ikipangwa na kuanza ugenini dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Manchester United imepangwa dhidi ya PSG katika hatua hiyo, ambapo itaanzia nyumbani. Michezo yote itapigwa katikati ya mwezi Februari mwakani.

Listi kamili ya droo hiyo ya 16 bora ya Klabu Bingwa Ulaya ni:

Schalke 04 Vs Man City, Atletico Madrid Vs Juventus, Man United Vs PSG Tottenham  Vs Dortmund, Lyon Vs Barcelona, Roma Vs FC Porto, Ajax Vs Real Madrid, Liverpool Vs Bayern.

Katika hatua nyingine, droo ya hatua ya 32 bora ya michuano ya Europa League imefanyika, ambapo klabu ya Genk ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ikipangiwa na Slavia Praha ya Jamhuri ya Czech.

Listi kamili ya droo hiyo ya hatua ya 32 bora ya michuano ya Europa League ni:

Viktoria Plzen Vs Dinamo Zagreb, Club Brugge Vs Red Bull Salzburg, SK Rapid Wien Vs Inter Milan, Slavia Praha Vs Genk, Krasnodar Vs Bayer Leverkusen, Zürich Vs Napoli, Malmö Vs Chelsea, Shakhtar Donetsk Vs Frankfurt, Fenerbahçe Vs Zenit, BATE Borisov Vs Arsenal, Lazio Vs Sevilla,  Rennes v Real Betis, Celtic vs Valencia, Sporting vs Villarreal, Galatasaray vs Benfica,  Olympiacos v Dynamo Kyiv.