Mchezaji aweka rekodi ya kucheza kwa miongo minne

Jumatatu , 6th Jan , 2020

Mcheza kikapu Vince Carter anayekipiga katika timu ya Atlanta Hawks inayoshiriki ligi ya NBA, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kucheza kwa miongo (decade) minne.

Vince Carter

Carter ameweka rekodi hiyo jana Jumapili wakati timu yake ya Atlanta Hawks ilipoifunga Indiana Pacers vikapu 116 kwa 111, ambapo Vince Carter alikuwa sehemu ya kikosi cha Atlanta.

Vince Carter mwenye miaka 42, alianza rasmi kucheza NBA mwaka 1999, ambapo baadhi ya nyota waliokuwa wakicheza wakati huo na sasa wamestaafu ni  Michael Jordan.

Katika kikosi cha Atlanta kuna wachezaji ambao wanacheza na Vince Carter lakini hawakuwa wamezaliwa wakati yeye anaanza kucheza NBA. Wachezaji hao ni Bruno Fernando, Trae Young, Kevin Huerter na Cam Reddish.

Vince Carter

Baadhi ya rekodi zake pamoja na tuzo.

Amecheza zaidi ya mechi 1,500 za NBA 

Ameingia mara 8 kwenye kikosi cha NBA All-Star

Pia amechukua medali ya dhahabu kwenye Olympic mwaka 2000.

Mchezaji mpya bora (NBA Rookie of the Year Award 1999)

Mchezaji wa kwanza mwenye miaka 40 kufunga pointi 3 kwenye mechi ya 'playoff' (April 22, 2017 vs. San Antonio Spurs, Western Conference 1st round).