Ijumaa , 31st Oct , 2014

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Boniface Wambura amesema wanasubiri ripoti ya Kamishna kuhusu tukio la mchezaji wa timu ya Temeke ya Tanzania Bara Said Mohamed kumjeruhi kwa kumachana na viwembe mchezaji wa timu ya Zanzibar

Mkurugenzi wa Mashindano,Boniface Wambura

Akizungumza na East Africa Radio, Wambura amesema tukio hilo ambalo lilitokea wakati wa kutafuta timu 16 bora zitakazoweza kucheza fainali za michuano hiyo ni la kusikitisha na kama ikithibitika ni kweli mchezaji huyo kafanya hili tukio hawatasita kumuwajibisha.

Wambura amesema mchezaji huyo atahukumiwa kwa sheria za soka kwani hairuhusiwi mchezaji kuingia na silaha aina yoyote wala kumjeruhi mchezaji au mtu yoyote, hivyo mchezaji huyo kama ametenda kosa hilo kweli atachukuliwa hatua kutokana na sheria.